Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Basi, Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu, hapo ndipo mtakapojua kwamba ‘Mimi Ndimi Niliye’, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Basi, Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu, hapo ndipo mtakapojua kwamba ‘Mimi Ndimi Niliye’, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Basi, Yesu akawaambia, “Mtakapokwisha mwinua Mwana wa Mtu, hapo ndipo mtakapojua kwamba ‘Mimi Ndimi Niliye’, na kwamba sifanyi chochote mimi mwenyewe, ila nasema tu yale Baba aliyonifundisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Kisha Isa akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua Mwana wa Adamu juu, ndipo mtajua kuwa mimi ndiye yule niliyesema, na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu, bali ninasema yale tu Baba yangu amenifundisha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Kisha Isa akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua juu Mwana wa Adamu, ndipo mtakapojua kuwa, ‘Mimi ndiye yule niliyesema na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu bali ninasema yale tu ambayo Baba yangu amenifundisha.

Tazama sura Nakili




Yohana 8:28
28 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi.


Mimi ndiye: na watadanganya wengi.


Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.


Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Tangu sasa nawaambieni kabla hayajatukia, illi yatakapotukia, mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.


kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;


illi neno lake Yesu litimizwe, alilolisema, akionyesha ni mauti gani atakayokufa.


wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja nae, huko na huko, na Yesu katikati.


Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali.


Na kama Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana buddi kuinuliwa:


Yesu akamwambia, Mimi nisemae nawe, ndiye.


Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.


Mimi siwezi kufanya neno kwa nafsi yangu: kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo, na hukumu yangu ina haki: kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake Baba aliyenipeleka.


Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka.


Bassi naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa kuwa msipoamini ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.


Hawakufahamu ya kuwa awatajia Baba.


Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Kabla Ibrahimu hajakuwapo, Mimi nipo.


Nao waliolipokea neno lake kwa furaha wakabatizwa: na siku ile wakazidishiwa watu wapata elfu tatu.


Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini: na hesabu ya watu ilikuwa kama elfu tano.


na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa ufufuo; Yesu Kristo Bwana wetu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo