Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 8:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Yesu alipozungumza nao tena, aliwaambia, “Mimi ndimi mwanga wa ulimwengu. Anayenifuata mimi hatembei kamwe gizani, bali atakuwa na mwanga wa uhai.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kisha Isa akasema nao tena, akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata, hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kisha Isa akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”

Tazama sura Nakili




Yohana 8:12
31 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kustirika ukiwa juu ya mlima.


Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.


Maadam mnayo nuru, iaminini nuru, mpate kuwa wana wa nuru. Hayo aliyasema Yesu, akaenda zake akajificha nao.


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Na hii ndiyo hukumu, ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, watu wakapenda giza zaidi ya nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.


Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.


Maadam nipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.


Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya mataifa, Upate kuwa wokofu hatta mwisho wa dunia:


ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa.


Hawa ni visiwa visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa:


Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;


Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;


ni mawimbi ya bahari vasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu, ni nyota zipoteazo, ambao giza ndio akiba yao waliowekewa milele.


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


Na mataifa wa hao wanaookolewa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa inchi wataleta utukufu wao na heshima yao ndani yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo