Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:39 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

39 Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 (Alisema hayo kumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watampokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 (Alisema hayo kumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watampokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 (Alisema hayo kumhusu Roho ambaye wale waliomwamini yeye watampokea. Wakati huo Roho alikuwa hajafika kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Isa aliposema haya, alimaanisha Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye wote waliomwamini wangempokea. Kwa maana hadi wakati huo Roho wa Mungu alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Isa alikuwa bado hajatukuzwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Isa aliposema haya alimaanisha Roho wa Mwenyezi Mungu ambaye wote waliomwamini wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Isa alikuwa bado hajatukuzwa.

Tazama sura Nakili




Yohana 7:39
42 Marejeleo ya Msalaba  

Wakasema, Wengine Yohana Mbatizaji, wengine Eliya, wengine Yeremia au mmojawapo wa manabii.


Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.


Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu.


Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:


Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.


Wakamwuliza, Nini bassi? U Eliya wewe? Akanena, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.


Wakamwuliza, wakimwambia, Mbona bassi wabatiza, kama wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?


Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu.


Mambo haya wanafunzi wake hawakuyafahamu hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walikumbuka ya kwamba ameandikiwa haya na ya kwamba walimtendea haya.


Yesu akajibu, akinena, Saa imefika, atukuzwe Mwana wa Adamu.


Na mkiomba lo lote kwa jina langu, hili nitalifanya, Baba atukuzwe ndani ya Mwana.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Yeye atanitukuza mimi: kwa kuwa atatwaa katika iliyo yangu, atawapasheni khabari.


Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu.


MANENO hayo aliyasema Yesu: akainua macho yake kuelekea mbinguni, akanena, Baba, saa ile imekuja. Mtukuze Mwana wako, illi Mwana wako nae akutukuze wewe;


Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu.


Akiisha kusema haya, akawapulizia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.


Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.


Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano.


Yesu akajibu, Nikijitukuza nafsi yangu, utukufu wangu si kitu; anitukuzae ni Baba yangu; mmnenae ninyi kuwa ni Mungu wenu.


akawauliza, Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hatta kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.


Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto:


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha mbalimbali, kama Roho alivyowajalia kutamka.


Mungu wa Ibrahimu na Isaak na Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambae ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.


Hatta walipokwisha kumwomba Mungu, pahali paie walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa uthabiti.


Lakini ikiwa Roho ya Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamfuati mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Lakini mtu aliye yote asipokuwa na Roho ya Kristo, huyo si mtu wake.


je! khuduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu?


Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo