Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Hatta siku ya mwisho, siku ile kubwa ya siku kuu, Yesu akasimama, akapaaza sauti yake, akinena, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalumu. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalumu. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Siku ya mwisho ya sikukuu hiyo ilikuwa siku maalumu. Yesu alisimama, akasema kwa sauti kubwa, “Aliye na kiu na aje kwangu anywe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Isa akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Isa akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.

Tazama sura Nakili




Yohana 7:37
50 Marejeleo ya Msalaba  

Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye mizigo nami nitawapumzisha.


Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti yake apigae mbin jangwani, Itengenezeni njia ya Bwana, Nyosheni mapito yake.


Wa kheri wenye njaa na kiu ya haki: maana hawo watashiba.


Akasema, Mimi ni sauti ya mtu apaazae sauti jangwani, Inyosheni njia ya Bwana! kama alivyonena nabii Isaya.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Yesu akajibu akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, nae ni nani akuambiae, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, nae angalikupa maji yaliyo hayi.


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea na kisima kinakwenda chini sana; bassi, umeyapata wapi haya maji yaliyo hayi?


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


wala hamtaki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima.


Yesu akawaambia, Mimi ni mkate wa uzima; yeye ajae kwangu hataona njaa kabisa, nae aniaminiye hataona kiu kamwe.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Kwa maima nyama yangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli,


Bassi Yesu akapaaza sauti yake hekaluni, akifundisha, akisema, Mimi mnanijua, na nitokako mnakujua; wala sikuja kwa naisi yangu, illa yeye aliyenipeleka ni wa kweli, msiyemjua ninyi.


Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.


wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho: kwa maana walikunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ni Kristo.


Vivi hivi nacho kikombe baada ya kula, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu: fanyeni liivi killa mnywapo, kwa ukumbusho wangu.


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Na Roho na Bibi arusi wasema, Njoo. Nae asikiae aseme, Njoo. Nae aliye na kiu, na aje: na apendae ayatwae maji ya uzima burre.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo