Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Viongozi wa Wayahudi wakasema wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi ambapo hatutaweza kumpata? Atakwenda kwa Wayahudi waliotawanyika kati ya Wagiriki, na kuwafundisha Wagiriki?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani?

Tazama sura Nakili




Yohana 7:35
29 Marejeleo ya Msalaba  

Na jina lake Mataifa watalitumainia.


Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Na palikuwa na Wayunani kadha wa kadha miongoni mwa watu waliopanda kwenda kuabudu wakati wa siku kuu.


NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.


Bassi Wayahudi wakanena, Je! atajiua, kwa kuwa anena, Niendako mimi hamwezi kuja?


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


Baadhi ya hao walikuwa watu wa Kupro na Kurene, nao walipofika Antiokia wakasema na Wahelenisti, wakakhubiri khabari njema za Bwana Yesu.


IKAWA huko Ikonio wakaingia pamoja katika sunagogi ia Wayahudi, wakanena; hatta jamaa kubwa ya Wayahudi na ya Wayunani wakaamini.


Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache.


Akatoa hoja zake katika sunagogi killa sabato akawavuta Wayahudi na Wayunani waamini.


Nao wameambiwa khabari zako, ya kwamba unawafundisha Wayahudi wote wakaao katika mataifa kumwacha Musa, ukiwaambia wasiwatahiri watoto wao, wala wasizifuate desturi.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


kwa maana siionci haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokofu, kwa killa aaminiye, kwa Myahudi kwanza, hatta kwa Myunani pia.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa.


YAKOBO, mtumwa wa Mungu, na Bwana Yesu Kristo, kwa kabila thenashara zilizotawanyika, salamu,


PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo