Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Bassi Yesu akanena, Bado muda kitambo nipo pamoja nanyi, kiisha nakwenda zangu kwake yeye aliyenipeleka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Yesu akasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Yesu akasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Yesu akasema, “Bado niko nanyi kwa muda mfupi, kisha nitamwendea yule aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Isa akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Isa akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili




Yohana 7:33
16 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo.


bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu,


Enyi watoto wachanga, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta: na kama nilivyowaambia Wayahudi, ya kama, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja: sasa nawaambia na ninyi.


Amin, amin, nawaambieni, Aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi na yeye atazifanya; atafanya na kubwa kuliko hizi, kwa kuwa nashika njia kwenda kwa Baba.


Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi.


Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Nakwenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi, kwa sababu nashika njia kwenda kwa Baba: kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.


kwa khabari ya haki, kwa sababu nakwenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;


Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba.


Lakini sasa nakwenda zangu kwake aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizae, Unakwenda zako wapi?


Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi.


Na sasa naja kwako; na haya nayasema ulimwenguni, illi wawe na furaha yangu imetimizwa ndani yao.


Yesu akamwambia, Usiniguse; kwa maana sijapaa kwa Baba yangu. Lakini enenda kwa ndugu zangu, ukawaambie, Ninapaa kwa Baba yangu na Baba yenu, kwa Mungu wangu na Mungu wenu.


Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo