Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Bassi ndugu lake wakamwambia, Ondoka bapa uende Yahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Basi, ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Basi, ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Basi, ndugu zake wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wazione kazi unazozifanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hivyo ndugu zake Isa wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hivyo ndugu zake Isa wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.

Tazama sura Nakili




Yohana 7:3
17 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae.


Jamaa zake walipopata khabari wakatoka kwenda kumkamata: maana walinena, Amerukwa na akili.


Wakaja mama yake na ndugu zake; wakasimama nje, wakamtuma mtu kumwita.


Mama yake na ndugu zake wakamwendea wala hawakuweza kumkaribia kwa sababu ya mkutano.


Akapewa khabari na watu, waliosema, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kukuona.


Yesu nae akaitwa pamoja na wanafunzi wake arusini.


Bassi watu wengi katika wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, Neno hili ni gumu, nani awezae kulisikia?


Kwa ajili ya haya wengi katika wanafunzi wake wakarejea nyuma, wala hawakuandamana nae tena.


Hatta ndugu zake walipokwisha kupanda, ndipo yeye nae akapanda kwenda kuishika siku kuu, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.


Kwa maana hakuna mtu afanyae neno kwa siri, na yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya haya, jidhihirishe kwa ulimwengu.


Maana hatta ndugu zake hawakumwamini.


Lakini Petro akasimama pamoja na wale edashara, akapaaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemi, jambo hili lijulike kwenu, mkasikilize maneno yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo