Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Na kumbe! ananena waziwazi wala hawamwambii neno? Yumkini wakuhwa wanajua kwa hakika ya kuwa huyu ni Kristo!

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Tazameni sasa! Anawaonya hadharani, wala hakuna mtu anayemwambia hata neno. Je, yawezekana kuwa viongozi wametambua kweli kwamba huyu ndiye Kristo?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Mbona yuko hapa anazungumza hadharani, na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Al-Masihi?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Mbona yuko hapa anazungumza hadharani na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Al-Masihi?

Tazama sura Nakili




Yohana 7:26
21 Marejeleo ya Msalaba  

Wakawatuma kwake wanafunzi wao pamoja na Maherodiano, wakanena, Mwalimu, twajua ya kuwa wewe u mtu wa kweli, ua njia va Mungu waifundisha katika kweli, wala hujali cheo cha mtu, kwa maana hutazami sura za watu.


Pilato akawaita pamoja makuhani wakuu, na wakubwa, na watu, akawaambia,


Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae.


Walakini hatta katika wakubwa wengi walimwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumwungama, wasije wakalolewa katika masunagogi.


Yesu akamjibu, Mimi nimesema na ulimwengu kwa wazi; mimi siku zote nalifundisha katika masunagogi na katika hekalu, wakusanyikapo Wayahudi siku zote; wala kwa siri sikusema neno.


PALIKUWA na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi;


Njoni, nitazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?


Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua?


Watu wengi katika makutano wakamwamini: wakasema, Atakapokuja Kristo, je! atafanya ishara nyingi zaidi kuliko hizi alizozifanya huyu?


Ni nani katika wakubwa amwammiye, au katika Mafarisayo?


Wazazi wake waliyasema haya kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi wamekwisha kuwafikana kwamba mtu akimwungama kuwa Kristo, ataharamishwa sunagogi.


Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Na walio wengi wa ndugu walio katika Bwana, wakipata kuthubutika kwa ajili ya kufungwa kwangu, wamezidi sana kuthubutu kulinena neno la Bwana pasipo khofu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo