Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Aliyewapeni torati si Musa? wala hapana mmoja wenu aitendae torati. Mbona mnatafuta kuniua?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Je, Mose hakuwapeni sheria? Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishika sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Je, Mose hakuwapeni sheria? Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishika sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Je, Mose hakuwapeni sheria? Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishika sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Je, Musa hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Je, Musa hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”

Tazama sura Nakili




Yohana 7:19
27 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Mafarisayo wakatoka wakamfanyia shauri la kumwangamiza.


Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.


Waandishi na makuhani wakini wakapata khabari wakatafuta jinsi ya kumwangamiza: maami walimwogopa, kwa sababu makutano yote walishangaa kwa elimu yake.


Akawaambia, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuokoa roho au kuua? Wakanyamaza.


marra wakaloka wale Mafarisayo, wakamfanyia shauri pamoja na Maherodiano jinsi ya kumwangamiza.


Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, neema na kweli zilikuwa kwa mkono wa Yesu Kristo.


Wakatafuta marra ya pili kumkamata: akatoka mikononi mwao.


Bassi tangu siku ile walifanya shauri wapate kumwua.


Kwa sababu hiyo Wayahudi wakaanza kumwudhi Yesu, wakitaka kumwua, kwa kuwa alitenda haya siku ya sabato.


Bassi kwa sababu hii Wayahudi wakazidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na haya alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.


Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba: yuko anaewashitaki, yaani Musa, mnaemtumaini ninyi.


NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.


Bassi baadhi ya watu wa Yerusalemi wakanena, Huyu si yeye wanaemtafuta illi kumwua?


Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema nae katika mlima Sinai, tena pamoja na baba zetu: ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.


Torali ni nini bassi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hatta mzao atakapokuja aliyepewa ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.


Kwa maana hatta wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sharia; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kujisifia miili yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo