Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Bassi Yesu akawajibu akasema, Elimu yangu siyo yangu, illa yake yeye aliyenipeleka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hapo Yesu akawajibu, “Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hapo Yesu akawajibu, “Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hapo Yesu akawajibu, “Mafundisho ninayofundisha si yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Ndipo Isa akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Ndipo Isa akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma.

Tazama sura Nakili




Yohana 7:16
14 Marejeleo ya Msalaba  

Huamini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu? Maneno niwaambiayo mimi, sisemi kwa shauri langu tu; lakini Baba akaae ndani yangu huzifanya kazi zake.


Asiyenipenda, hayashiki maneno yangu; na neno mnalolisikia silo langu, bali lake Baba aliyenipeleka.


Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu uliwachukia, kwa kuwa wao si watu wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Amin, amin, nakuambia, Tulijualo twalisema, na tuliloliona twalishuhudu; na ushuhuda wetu hamwukubali.


Ajae kutoka juu huyu yu juu ya yote: aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, na anena mambo ya dunia: yeye ajae kutoka mbinguni yu juu ya yote.


Mimi siwezi kufanya neno kwa nafsi yangu: kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo, na hukumu yangu ina haki: kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake Baba aliyenipeleka.


Hakuna mtu awezae kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka: nami nitamfufua siku ya mwisho.


Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.


Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo