Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 7:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Kulikuwa na minongono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Kulikuwa na minongono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Kulikuwa na minong'ono mingi katika umati wa watu. Baadhi yao walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “La! Anawapotosha watu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Isa katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Isa katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 7:12
20 Marejeleo ya Msalaba  

Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebul, je, si zaidi wale walio nyumbani mwake?


Nao walipotafuta kumkamata, wakawaogopa makutano, kwa maana walimwona kuwa nabii.


wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.


Yesu akamwambia, Mbona waniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja ndiye Mungu.


Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.


Akatoka mtu, jina lake Yusuf, nae ni mtu wa baraza yao, mtu mwema, mwenye haki


Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa lililo jema: na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa lililo ovu: kwa sababu kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.


Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.


Mafarisayo wakawasikia makutano wakinungʼunika hivi kwa khabari zake: bassi Mafarisayo na makuhani wakuu wakatuma watumishi illi wamkamate.


Bassi Mafarisayo wakawajibu, Je! ninyi nanyi mmedanganyika?


Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.


Bassi baadhi ya Mafarisayo wakanena, Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakanena, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?


Maana alikuwa mtu mwema, amejaa Roho Mtakatifu na imani: watu wengi wakajitia upande wa Bwana.


Kwa maana ni shidda mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki, illakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema.


Yatendeni mambo yote pasipo manungʼuniko na mashindano,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo