Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 6:62 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

62 Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

62 Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

62 Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

62 Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

62 Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

62 Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza?

Tazama sura Nakili




Yohana 6:62
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


Bassi Bwana, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu.


Ikawa katika kuwabariki, akajitenga nao, akachukuliwa juu mbinguni.


Nalitoka kwa Baba, nimekuja ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu, nashika njia kwenda kwa Baba.


Na mimi simo tena ulimwenguni, na hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba mtakatifu, uwalinde kwa jina lako wale ulionipa; wawe moja, kama sisi.


Na hapana mtu aliyepanda mbinguni, illa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, Mwana wa Adamu alioko mbinguni.


Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.


Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?


Bassi Yesu akawaambia, Amin, amin, nsiwaambieni. Msipoila nyama yake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani jemi.


Akiisha kusema haya, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.


alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo