Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 6:57 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

57 Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

57 Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

57 Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

57 Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.

Tazama sura Nakili




Yohana 6:57
19 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Bado kidogo na ulimwengu haunioni tena; bali ninyi mnaniona; kwa sababu mimi ni hayi, ninyi nanyi mtakuwa hayi.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake;


Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae.


Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka.


Kwa kuwa katika Adamu wote wanakufa, kadhalika na katika Kristo wote watahuishwa.


Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza Adamu alikuwa nafsi hayi; Adamu wa mwisho roho yenye kuhuisha.


Maana, ijapokuwa alisulibiwa katika udhaifu, illakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; bali tutaishi pamoja nae kwa uweza wa Mungu ulio ndani yenu.


Nimesulibiwa pamoja na Kristo, illakini ni hayi; wala si mimi tena, bali Kristo yu hayi ndani yangu; na uhayi nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu aliyenipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.


Maana wao wenyewe wanatangaza khabari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu, mkaziacha sanamu illi kumtumikia Mungu aliye hayi, wa kweli,


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo