Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 6:45 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

45 Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Bassi killa aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 Manabii wameandika: ‘Watu wote watafundishwa na Mungu.’ Kila mtu anayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake, huja kwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 Manabii wameandika: ‘Watu wote watafundishwa na Mungu.’ Kila mtu anayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake, huja kwangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 Manabii wameandika: ‘Watu wote watafundishwa na Mungu.’ Kila mtu anayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake, huja kwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu.

Tazama sura Nakili




Yohana 6:45
24 Marejeleo ya Msalaba  

Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


kama ilivyoandikwa katika chuo cha manabii, Angalia, mimi namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, Atakaefanyiza njia yako mbele yako.


(Kama alivyosema kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu mwanzo),


Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii.


Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata;


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Akanena, Kwa sababu hii nimewaambia ya kwamba hapana mtu awezae kuja kwangu, isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.


Angalieni, bassi, isije khabari ile iliyonenwa katika manabii,


Bassi Mungu akaghairi, akawaacha, wakaliabudu jeshi la mbinguni, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha manabii, Je! mlinitolea dhabihu na sadaka Miaka arubaini katika jangwa, enyi nyumba ya Israeli?


Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awapeni roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye:


Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo.


Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo.


Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo