Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 6:39 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

39 Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: Nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: Nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Haya ndio mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Haya ndiyo mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho.

Tazama sura Nakili




Yohana 6:39
29 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.


Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni mmoja wa wadogo hawa apotee.


Msiogope, enyi kundi dogo, kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapeni ufalme.


Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.


Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; wahkuwa wako, ukanipa mimi: na neno lako wamelishika.


Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako.


illi litimizwe lile neno alilolisema, Hawa ulionipa sikupoteza hatta mmoja wao.


Msistaajabie haya: kwa maana saa inakuja, ambayo watu wote waliomo makaburini watakapoisikia sauti yake, nao watatoka:


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Hakuna mtu awezae kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka: nami nitamfufua siku ya mwisho.


Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu ana uzima wa milele; mimi nitamfufua siku ya mwisho.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Na Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua na sisi kwa uweza wake.


Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.


Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; na kama amefanya dhambi, atasamehewa.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo