Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 6:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Yesu akawajibu, akasema, Amin, amin, nawaambieni, Mnanitafuta, si kwa sababu mliona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate, mkashiba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Isa akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Isa akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.

Tazama sura Nakili




Yohana 6:26
20 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.


Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.


Bassi Yesu, akitambua ya kuwa walitaka kuja kumchukua illi wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani, yeye peke yake.


Makutano mengi wakamfuata, kwa sababu waliziona ishara alizowafanyia wagonjwa.


bassi makutano walipoona ya kuwa Yesu hakuwako huko wala wanafunzi wake, wenyewe wakaingla vyomboni, wakaenda Kapernaum wakimtafuta Yesu.


Wakamwambia, Unafanya ishara gani bassi illi tuone tukaamini? Unatenda kazi gani?


Lakini naliwaambieni ya kwamba mmeniona bila kuniamini.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi ana uzima wa milele.


Bassi Yesu akawaambia, Amin, amin, nsiwaambieni. Msipoila nyama yake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani jemi.


Lakini kuna wengine miongoni mwemi wasioamini. Maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini na ni nani atakaenisaliti.


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Yesu Kristo.


mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo