Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Kwa maana kuna wakati malaika hushuka akaiingia ile birika, akayatibua maji: bassi yeye aliyeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, akaponea ugonjwa wote uliokuwa umempata.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 maana mara kwa mara malaika alishuka majini nyakati fulani na kuyatibua. Mtu yeyote aliyekuwa wa kwanza kuingia majini baada ya maji kutibuliwa, alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao.]

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 maana mara kwa mara malaika alishuka majini nyakati fulani na kuyatibua. Mtu yeyote aliyekuwa wa kwanza kuingia majini baada ya maji kutibuliwa, alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao.]

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule angekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao].

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao].

Tazama sura Nakili




Yohana 5:4
18 Marejeleo ya Msalaba  

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hatta leo ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.


Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu, na haki yake; na haya yote mtazidishiwa.


Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba; kwa maana nawaambieni ya kwamba watu wengi watatafuta kuingia nao bawataweza.


Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.


Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, na waliopooza, wakingoja maji yachemke.


Na huko palikuwa na mtu, amekuwa hawezi muda wa miaka thelathini na minane.


Yule mgonjwa akamjibu, Bwana, sina mtu wa kunitia birikani, maji yanapotibuliwa; bali wakati ninapokuja mimi, mtu mwingine hushuka mbele yangu.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo