Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:39 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

39 Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Nyinyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uhai wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Nyinyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uhai wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Nyinyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uhai wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele. Maandiko haya ndio yanayonishuhudia mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.

Tazama sura Nakili




Yohana 5:39
51 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajihu, akawaamhia, Mwajidanganya, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.


Nae akajibu, akawaambia, Musa aliwaamuru nini?


Hatta andiko hili hamjalisoma? Jiwe walilokataa waashi Hili limekuwa jiwe kuu la pembeni.


Ibrahimu akasema, Wana Musa na manabii; wawasikilize wao.


Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa.


Nae akawaambia, Enyi wapumbavu, na wenye mioyo mizito katika kuyaamini yote waliyoyasema manabii!


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti


Yuko mwingine anaenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.


Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.


wala hamtaki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima.


Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; maana yeye aliandika khahari zangu.


Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.


Kwa maana wakaao Yerusalemi, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua huyu, wala sauti za manabii wanaosomwa killa sabato, wamezitimiza kwa kumhukumu.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Mfalme Agrippa, wawaamini manabii? Najua ya kuwa wawaamini.


ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,


Kwafaa sana kwa killa njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


Lakini sasa waitamani inchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.


Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa: na wengine walibanwa, wasiukubali ukombozi, wapate ufufuo ulio bora:


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo