Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Nae Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nyinyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nyinyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nyinyi hamjapata kamwe kusikia sauti yake, wala kuuona uso wake,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake,

Tazama sura Nakili




Yohana 5:37
20 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.


sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwana wangu mpendwa, ndiwe unipendezae.


Akaanza toka Musa na manabii, akawafasiria katika maandiko yote mambo yaliyomkhusu yeye.


Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Yesu akamwambia, Nimekuwa pamoja nanyi siku hizi zote wala hukunijua, Filipo? Aliyeniona mimi, amemwona Baba; wasemaje wewe, Tuonyeshe Baba?


Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.


Yuko mwingine anaenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.


Msikitendee kazi chakula chenye kuharibika, bali chakula kidumucho hatta uzima wa milele, Mwana wa Adamu atakachowapeni: maana huyu ndiye aliyetiwa muhuri na Baba, yaani, Mungu.


Mimi ndimi ninaejishuhudia nafsi yangu, nae Baba aliyenipeleka ananishuhudia.


Kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu wa hekima peke yake, kwake yeye heshima na utukufu milele na milele. Amin.


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


Tukiupokea ushuliuda wa wana Adamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwana wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo