Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:36 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

36 Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Lakini mimi nina ushahidi juu yangu ambao ni mkuu zaidi kuliko ule wa Yohane. Kwa maana kazi ninazofanya, kazi alizonipa Baba nizifanye, ndizo zinazonishuhudia kwamba Baba ndiye aliyenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 “Ninao ushuhuda mkuu kuliko ule wa Yahya. Kazi ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, kazi hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba amenituma.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 “Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yahya. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma.

Tazama sura Nakili




Yohana 5:36
17 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akajibu akawaambia, Enendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona:


Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwa katika nyumba ya baba yangu?


Yesu akawajibu, Naliwaambieni, nanyi hamwamini; kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu, ndizo zinazonishuhudia.


Bali wengine walisema, Je! huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?


Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.


Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza.


Hatta alipokuwapo Yerusalemi wakati wa Pasaka katika siku kuu, watu wengi wakaliamini jina lake, wakiona ishara zake alizozifanya.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.


Yuko mwingine anaenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Tukiupokea ushuliuda wa wana Adamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, amemshuhudia Mwana wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo