Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Ndani ya hayo jamii kubwa ya wagonjwa walikuwa wamelala, vipofu, viwete, na waliopooza, wakingoja maji yachemke.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Humo barazani mlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: Vipofu, viwete na waliopooza. [Walikuwa wakingojea maji yatibuliwe,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Humo barazani mlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: Vipofu, viwete na waliopooza. [Walikuwa wakingojea maji yatibuliwe,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Humo barazani mlikuwa na wagonjwa wengi wamekaa: vipofu, viwete na waliopooza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe.

Tazama sura Nakili




Yohana 5:3
12 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamwendea makutano mengi walio na viwete, vipofu, bubu, vilema, na wengine wengi pamoja nao, wakawaweka miguuni pa Yesu; akawaponya;


Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema:


Na huko Yerusalemi penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiehrania Bethesda, nayo ina matao matano.


Kwa maana kuna wakati malaika hushuka akaiingia ile birika, akayatibua maji: bassi yeye aliyeingia kwanza baada ya maji kutibuliwa, akaponea ugonjwa wote uliokuwa umempata.


Bali tukikitumaini kitu tusichokiona, twakingojea kwa uvumilivu.


Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo