Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 “Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 “Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 “Kweli nawaambieni, anayesikia neno langu, na kumwamini yule aliyenituma, anao uhai wa milele. Hatahukumiwa kamwe, bali amekwisha pita kutoka kifoni na kuingia katika uhai.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 “Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 “Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani.

Tazama sura Nakili




Yohana 5:24
28 Marejeleo ya Msalaba  

Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


na killa mwenye uzima na kuniamini mimi hatakufa kabisa hatta milele. Je! waamini haya?


Yesu akapaaza sauti yake akasema, Aniaminiye mimi, haniamini mimi, bali yeye aliyenipeleka.


lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu.


Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; na asiyemtii Mwana hataona uzima, hali ghadhabu ya Mungu inamkalia.


Avunae hupokea mshahara na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, illi yeye apandae na yeye avunae wafurahi pamoja.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi ana uzima wa milele.


Huu ni mkate ushukao kutoka mbinguni, illi mtu aule wala asife.


Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.


Huu ni mkale ulioshuka kutoka mbinguni; si kama baba zenu walivyoila manna wakafa; aulae mkate huu ataishi milele.


Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


ambae kwa yeye mlimwamini Mungu, aliyemfufua akampa utukufu; hatta imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo