Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Maana Baba ampenda Mwana, amwonyesha yote ayatendayo mwenyewe; na kazi kubwa zaidi kuliko hizi atamwonyesha illi ninyi mpate kustaajabu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Baba ampenda Mwana, na humwonesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Baba ampenda Mwana, na humwonesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Baba ampenda Mwana, na humwonesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Baba ampenda Mwana na kumwonesha yale ambayo yeye Baba mwenyewe anayafanya, naye atamwonesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Baba ampenda Mwana na kumwonyesha yale ambayo yeye Baba mwenyewe anayafanya, naye atamwonyesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa.

Tazama sura Nakili




Yohana 5:20
17 Marejeleo ya Msalaba  

Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu: wala hakuna mtu amjuae Mwana, illa Baba; wala hakuna mtu amjuae Baba illa Mwana, na ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.


Tena Shetani akamchukua hatta mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fakhari yake, akamwambia,


Akawagenkia wanafunzi wake akasema, Nimekahidhiwa vyote na Baba yangu: wala hapana mtu ajuae khabari za Mwana illa Baba: wala khabari za Baha illa Mwana, na mtu ye yote ambae Mwana apenda kumfunulia.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe?


Amin, amin, nawaambieni, Aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi na yeye atazifanya; atafanya na kubwa kuliko hizi, kwa kuwa nashika njia kwenda kwa Baba.


Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyosikia kwa Baba nimewaarifuni.


Naliwajulisiia jina lako, tena nitawajulisha, illi pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, na mimi niwe ndani yao.


Baba ampenda Mwana, amempa vyote mikononi mwake.


Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao.


Amin, amin, nawaambieni, Saa inakuja, na sasa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wale waisikiao watakuwa hayi.


wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliofanya manyonge kwa ufufuo wa hukumu.


Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, ya kama, Huyu ndiye mwanangu nimpendae, amhae nimependezwa nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo