Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 5:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Bassi Yesu akajibu, akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Mwana hawezi kutenda neno kwa nafsi yake, illa lile amwonalo Baba analitenda; kwa maana yote atendayo yeye, hayo na Mwana ayatenda vilevile.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake. Yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake, yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo.

Tazama sura Nakili




Yohana 5:19
43 Marejeleo ya Msalaba  

Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu.


Kwa maana mimi sikusema kwa nafsi yangu tu; bali yeye aliyenipeleka, yaani Baba, ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.


Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele: bassi haya ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.


Huamini ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba ndani yangu? Maneno niwaambiayo mimi, sisemi kwa shauri langu tu; lakini Baba akaae ndani yangu huzifanya kazi zake.


Yesu akajibu, akawaambia, Livunjeni hekalu hii, nami kwa siku tatu nitaisimamisha.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha awatakao.


Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka.


Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.


Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi.


Mungu akamfufua, akilegeza utungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Bassi tulizikwa pamoja nae kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tutembee katika upya wa uzima.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


Bassi, ikiwa Kristo amekhubiriwa kwenu ya kwamba amefufuka, mbona wengine wenu wasema kwamba hakuna kiyama ya wafu?


tukijua kama yeye aliyemfufua Bwana Yesu atatufufua na sisi pamoja na Yesu, na kutuhudhurisha pamoja nanyi.


Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu ya Kristo, illi killa mtu apokee kadiri alivyotenda kwa mwili, vikiwa vyema au vikiwa vibaya.


hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);


awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho yake, katika mtu wa ndani;


atakaeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule awezao kuvitiisha hatta na vitu vyote chini yake.


Nayaweza mambo yote katika yeye anitiae nguvu.


mkiwezeshwa kwa nwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya killa namna na uvumilivu pamoja na furaha;


Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya inchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni viti vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake,


Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja nae.


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


nami nitawaua watoto wake kwa manti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzae viuno na mioyo. Nami nitampa killa mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo