Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 4:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Bassi yule mwanamke wa Kisamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke wa Kisamaria? kwa maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe nikupe maji ya kunywa?” Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.

Tazama sura Nakili




Yohana 4:9
12 Marejeleo ya Msalaba  

Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie:


Lakini Msamaria mmoja akisafiri, akamjia, nae alipomwona akamhurumia;


Marra hiyo wakaja wanafunzi wake wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hapana aliyesema, Unatafuta nini? au, Kwa nini unasema nae?


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.


Akawaambia, Mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi aongee na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, hikini Mungu amenionya, nisimwite mtu awae yote mchafu wala najis.


Bassi, tuma watu kwenda Yoppa, ukamwite Simon aitwae Petro, aje hapa; anakaa katika nyumha ya Simon, mtengenezaji wa ngozi, karibu ya pwani: nae akija atasema nawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo