Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 4:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Bassi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Ilikuwa yapata saa sita.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kisima cha Yakobo kilikuwa huko. Naye Isa alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Huko ndiko kulikokuwa na kile kisima cha Yakobo. Naye Isa alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.

Tazama sura Nakili




Yohana 4:6
12 Marejeleo ya Msalaba  

Tangu saa sita palikuwa giza juu ya inchi yote hatta saa tissa.


Akafunga siku arubaini mchana na usiku, baadae akaona njaa.


Kukawa msukosuko mkuu baharini, hatta chombo kikafunikizwa na mawimbi: nae alikuwa amelala.


Akamzaa mtoto wake wa kifungua mimba, akamfunga nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakuona nafasi katika nyumba ya wageni.


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vioto vyao, bali Mwana wa? Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.


Yesu akajibu, Saa za mchana je si thenashara? Mtu akienda mchana hajikwai, kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu.


Je! wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki, nae mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na nyama zake?


Bassi akafika mji wa Samaria, uitwao Sukar, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusuf mwanawe.


Akaja mwanamke wa Kisamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo