Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 4:48 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

48 Bassi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Yesu akamwambia, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Yesu akamwambia, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Yesu akamwambia, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 Isa akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

48 Isa akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”

Tazama sura Nakili




Yohana 4:48
29 Marejeleo ya Msalaba  

WAKAMJIA Mafarisayo na Masadukayo, wakamjaribu, wakamwomba awaonyeshe ishara itokayo mbinguni.


Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


Aliponya watu wengine, hawezi kujiponya nafsi yake. Akiwa mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani, naswi tutamwamini.


kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.


Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni.


Akamwambia, Wasiposikia Musa na manabii, ajapoondoka mtu katika wafu, hawatashawishwa.


Lakini ijapokuwa amefanya ishara kubwa namna hii mbele yao, hawakumwamini;


Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.


Bassi Wayahudi wakajibu wakamwambia, Ishara gani utuonyeshayo, iwapo unafanya haya?


Yesu amwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini; wa kheri wasioona wakaamini.


Yule diwani akamwambia, Bwana, shuka kabla hajafa mtoto wangu.


Bassi wakakaa huko wakati mwingi, wakinena kwa uthabiti katika Bwana, aliyelishuhudia neno la neema yake, akiwajalia ishara na maajabu yatendeke kwa mikono yao.


Bassi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paolo wakiwapasha khabari za ishara na maajabu ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika mataifa.


Nitatoa ajabu katika mbingu juu, Na ishara katika inchi chini, Damu na moto, na mvuke wa moshi:


Enyi waume wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;


Killa mtu akaingiwa na khofu: ajabu nyingi na ishara zikafanyika kwa ujumbe wa mitume.


ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.


Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara na maajabu mengi katika watu: nao wote walikuwa kwa nia moja katika ukumbi wa Sulemani:


Na Stefano, akijaa imani na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.


Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika inchi ya Misri, na katika bahari ya Sham, na katika jangwa muda wa miaka arubaini.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima;


Maana ishara za mtume zilitendwa kati yenu katika uvumilivu wote, kwa ishara na maajabu na nguvu.


ambae kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kazi kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za nwongo,


Mungu nae akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa karama za Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo