Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 4:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako; maana tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika yake huyu ni Mwokozi wa ulimwengu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kwamba huyu ndiye Al-Masihi, Mwokozi wa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Al-Masihi, Mwokozi wa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 4:42
23 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atazaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, ndiye atakaewaokoa watu wake na dhambi zao.


Nuru ya kuwaangaza mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Bassi alipofika Yesu, akamkuta amekwisha kuwa kaburini yapata siku nne.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Njoni, nitazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! haimkini huyu kuwa ndiye Kristo?


Watu wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.


Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani Yesu, kama alivyoahidi,


Wala hakuna wokofu katika mwingine aliye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wana Adamu litupasalo kuokolewa nalo.


Mtu kuyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toha na masamaha ya dhambi.


yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; nae ametia ndani yetu neno la upatanisho.


Kwa maana twajitaabisha na kujitahidi katika jambo hili, kwa sababu twamtumaini Mungu aliye hayi aliye mwokozi wa watu wote, khassa wa hao waaminio.


nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.


Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo