Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 4:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Lakini Isa akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Lakini Isa akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.

Tazama sura Nakili




Yohana 4:34
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akiomba, akinena, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kinipitie; walakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.


Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha.


Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake.


Kadhalika nawaambia ninyi, iko furaha mbele ya malaika zake Mungu kwa mwenye dhambi mmoja atubuye.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.


Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwa katika nyumba ya baba yangu?


Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza.


Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu.


Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho.


Akawaambia, Mimi nina chakula msichokijua ninyi.


Mimi siwezi kufanya neno kwa nafsi yangu: kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo, na hukumu yangu ina haki: kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake Baba aliyenipeleka.


Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.


Kwa maana mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.


Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka.


Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo.


Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo