Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 3:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Isa akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia ufalme wa Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Isa akamwambia, “Amin, amin nakuambia, hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia Ufalme wa Mwenyezi Mungu kama hajazaliwa kwa maji na kwa Roho.

Tazama sura Nakili




Yohana 3:5
35 Marejeleo ya Msalaba  

akasema, Amin, nawaambieni, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kabisa katika ufalme wa mbinguni.


Nawaambieni tena, Ni rakhisi ngamia kupenya katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.


Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.


Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Maana nawaambieni, Haki yenu isipozidi kuliko haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.


Lakini Yesu alipoona akachukiwa sana, akawaambia, Waacheni watoto wachanga waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawo ufalme wa mbinguni ni wao.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


Na jicho lako likikukosesha, litupe: ni kheri kuingia katika ufalme wa Mungu, una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehannum ya moto:


Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba; kwa maana nawaambieni ya kwamba watu wengi watatafuta kuingia nao bawataweza.


Nawaambieni sivyo: lakini msipotuhu nyote mtaangamia vivyo hivyo.


Nawaanibieni, Sivyo: lakini msipotubu, nyote mtaangamia vivyo hivyo.


waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Nikodemo amwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mama yake marra ya pili akazaliwa?


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:


Maana ufalme wa Muugu si kula na kunywa, bali baki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Nisemayo ni haya, ndugu, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharihika.


Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


kama vile Mungu alivyotangulia kuwajua tangu milele katika utakaso wa Roho, hatta wakapata kutii na kunyunyizwa damu ya Yesu Kristo; Neema na amani ziongezwe kwenu.


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo