Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 3:36 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

36 Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; na asiyemtii Mwana hataona uzima, hali ghadhabu ya Mungu inamkalia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

36 Anayemwamini Mwana anao uhai wa milele; asiyemwamini Mwana hatakuwa na uhai wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

36 Anayemwamini Mwana anao uhai wa milele; asiyemwamini Mwana hatakuwa na uhai wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

36 Anayemwamini Mwana anao uhai wa milele; asiyemwamini Mwana hatakuwa na uhai wa milele, bali ghadhabu ya Mungu hubaki juu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

36 Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

36 Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mwenyezi Mungu itakuwa juu yake.”

Tazama sura Nakili




Yohana 3:36
38 Marejeleo ya Msalaba  

Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


Kwa kuwa macho yangu yamenona wokofu wako,


Na wote wenye mwili watanona wokofu wa Mungu.


Bali wote waliompokea aliwapa mamlaka ya kufanyika watoto wa Mungu, ndio waliaminio jina lake:


nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Avunae hupokea mshahara na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, illi yeye apandae na yeye avunae wafurahi pamoja.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Huu ni mkale ulioshuka kutoka mbinguni; si kama baba zenu walivyoila manna wakafa; aulae mkate huu ataishi milele.


Amin, amin, nawaambieni, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti kabisa hatta milele.


Walakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.


Kwa sababu sharia ndiyo ifanyayo hasira; maana pasipo sharia, hapana kosa.


Bassi zaidi sana tukiisha kupewa haki katika damu yake tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye.


SASA, bassi, hapana hukumu juu yao walio katika Kristo Yesu, wasioenenda kwa kufuata mambo ya mwili bali mambo ya roho.


Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sharia, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu asiodumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sharia, ayafanye.


Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi.


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


Kwa kuwa Mungu hakutuweka kwa hasira vake bali tupate wokofu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo,


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Na ni nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika raha yake, illa wale wasioamini?


Bassi twaona ya kuwa bawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo