Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 3:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Yule aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, maana Mungu humjalia mtu huyo Roho wake bila kipimo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humpa Roho wake pasipo kipimo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Yeye aliyetumwa na Mwenyezi Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo.

Tazama sura Nakili




Yohana 3:34
29 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua; Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae; Nitamtia roho yangu, Nae atuwatangazia Mataifa hukumu.


Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,


Na katika ujazi wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.


Lakini ajapo Mfariji, nitakaewapelekea toka kwa Baba, Roho ya kweli atokae kwa Baba, yeye atanishuhudia.


Lakini mimi nawaambieni iliyo kweli; Yawafaa ninyi mimi niondoke: kwa maana nisipoondoka, Mfariji hatakuja kwenu; bali nikienda zangu, nitampeleka kwenu.


Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.


Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake;


Bassi Yesu akawajibu akasema, Elimu yangu siyo yangu, illa yake yeye aliyenipeleka.


Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu niliyewaambia kweli ile niliyoisikia kwa Baba yangu. Ibrahimu hakufanya hivi. Ninyi nmazitenda kazi za baba yenu.


Aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; kwa hiyo ninyi hamsikii, kwa sababu ninyi si wa Mungu.


hatta siku ile alipowaagiza kwa Roho Mtakatifu mitume aliowachagua, akachukuliwa juu:


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


Kwa sababu sharia ya Roho ya uzima ule ulio katika Yesu Kristo imeniacha huru, nikawa mbali ya sharia ya dhambi na mauti.


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


Kwa kuwa katika yeye ilipendeza utimilifu wote ukae,


Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa namna ya kimwili.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa mwenye kin maji ya chemchemi ya maji ya uzima, burre.


AKANIONYESHA mto wa maji ya uzima, wenye kungʼaa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo