Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 3:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 Ajae kutoka juu huyu yu juu ya yote: aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, na anena mambo ya dunia: yeye ajae kutoka mbinguni yu juu ya yote.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia. Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia. Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Anayekuja kutoka juu ni mkuu kuliko wote; atokaye duniani ni wa dunia, na huongea mambo ya kidunia. Lakini anayekuja kutoka mbinguni ni mkuu kuliko wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote.

Tazama sura Nakili

Yohana 3:31
22 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia.

Yohana akamshuhudia, akapaaza sauti yake, akinena, Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, kwamba, Ajae nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.

Ndiye ajae nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, wala mimi sistahili niilegeze gidam ya kiatu chake.

Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, Yuaja mtu nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, kwa maana alikuwa kabla yangu.

Yeye hana buddi kuzidi, bali mimi kupungua.

Kwa maana mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.

Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Akawaambia, Ninyi wa chini, mimi wa juu; ninyi wa ulimwengu huu, mimi si wa ulimwengu huu.

Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akikhubiri amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),

na katika bao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili, aliye juu ya mambo yote, Mungu, anaehimidiwa milele. Amin.

BASSI hatta agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidumia.

alioko mkono wa kuume wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zimetiishwa chini yake.

Hawo ni wa dunia; kwa biyo wanena ya dunia, dunia ikawasikia.

Nae ana jina limeandikwa katika vazi lake mi paja vake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo