Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 3:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabbi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ngʼambu ya Yardani, uliyemshuhudia wewe, huyu nae anabatiza, na watu wote wanamwendea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Basi, wanafunzi hao wakamwendea Yohane na kumwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ngambo ya Yordani na ambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watu wote wanamwendea.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Basi, wanafunzi hao wakamwendea Yohane na kumwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ngambo ya Yordani na ambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watu wote wanamwendea.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Basi, wanafunzi hao wakamwendea Yohane na kumwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani na ambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watu wote wanamwendea.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Wakamwendea Yahya wakamwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Wakamwendea Yahya wakamwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng’ambo ya Mto Yordani, yule uliyeshuhudia habari zake, sasa anabatiza na kila mtu anamwendea!”

Tazama sura Nakili




Yohana 3:26
23 Marejeleo ya Msalaba  

na kusalimiwa sokoni, na kuitwa na watu, Rabbi, Rabbi.


Bali ninyi nisiitwe Rabbi; maana mwalimu wenu yu mmoja ndiye Kristo, na ninyi nyote ni ndugu.


Yohana akamshuhudia, akapaaza sauti yake, akinena, Huyu ndiye niliyemnena khabari zake, kwamba, Ajae nyuma yangu amekuwa mbele yangu; kwa maana alikuwa kabla yangu.


Huyu alikuja kwa ushuhuda, illi aishuhudie nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.


Kulikuwako nuru halisi, imtiayo nuru killa mtu ajae katika ulimwengu.


Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini: na Warumi watakuja, wataondoa mahali petu na taifa letu.


Bassi Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, Mwaona kwamba hamfai neno: tazameni, ulimwengu umekwenda nyuma yake.


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


BASSI Bwana alipojua ya kuwa Mafarisayo wamesikia kwamba Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kubatiza,


(lakini Yesu mwenyewe hakuhatiza, hali wanafunzi wake),


Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabbi, ule.


Ninyi mlituma watu kwa Yohana, akaishuhudia kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo