Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 3:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Maana Mungu hakumpeleka Mwana wake ulimwenguni auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa.

Tazama sura Nakili




Yohana 3:17
36 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, mwanamke bikira atachukua mimba, nae atazaa mwana, Na watamwita jina lake Immanuel; tafsiri yake, Mungu kati yetu.


Angalieni msidharau mmoja wa wadogo hawa; kwa maana nawaambieni ya kwamba malaika zao mbinguni siku zote wanamtazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.


Maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za wana Adamu, bali kuziokoa. Wakaenda zao hatta mji mwingine.


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


je! yeye ambae Baba alimtakasa akamtuma ulimwenguni, ninyi mwamwambia, Unakufuru, kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?


Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni.


Wote wawe umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, na mimi ndani yako, illi na hawa wawe umoja ndani yetu: ulimwengu upate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.


mimi ndani yao, na wewe ndani yangu, wapate kukamilika na kuwa umoja; illi ulimwengu ujue ya kuwa udiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; wakavapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakaamini ya kwamba ndiwe uliyenituma.


Bassi Yesu akawaambia marra ya pili, Amani kwenu; kama Baba alivyonipeleka, nami nawatuma ninyi.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


Lakini ushuhuda nilio nao ni mkubwa kuliko ule wa Yohana: kwa kuwa zile kazi nilizopewa na Baba nizimalize, kazi hizo zenyeye ninazozitenda zinanishuhudia kwamba Baba amenituma.


Na neno lake hamnalo likikaa ndani yenu, kwa kuwa ninyi hamwamini yeye alivetumwa nae.


Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba: yuko anaewashitaki, yaani Musa, mnaemtumaini ninyi.


Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae.


Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu.


Lakini mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, nae ndiye aliyenituma.


Akamwambia, Hapana Bwana. Yesu akamwambia, Nami sikuhukumu. Enenda, wala usitende dhambi tena.


Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.


nae ni kipatanisho kwa dhambi zetu: wala si kwa dhambi zetu tu, bali kwa dhambi za ulimwengu wote.


Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo