Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 3:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na hapana mtu aliyepanda mbinguni, illa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, Mwana wa Adamu alioko mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu, ambaye ameshuka kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu, ambaye ameshuka kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu, ambaye ameshuka kutoka mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Hakuna mtu yeyote aliyeenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Hakuna mtu yeyote aliyekwenda mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, yaani, Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili




Yohana 3:13
24 Marejeleo ya Msalaba  

mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.


bassi Yesu akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu, na anakwenda kwa Mungu,


Na sasa unitukuze wewe, Baba, pamoja nawe, kwa utukufu nle niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya kuwako ulimwengu.


Ikiwa nimewaambia mambo ya duniani, nanyi hamwa, mini, mtaaminije, niwaambiapo mambo ya mbinguni?


Ajae kutoka juu huyu yu juu ya yote: aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, na anena mambo ya dunia: yeye ajae kutoka mbinguni yu juu ya yote.


Kwa maana mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.


Kwa kuwa sikushuka kutoka mbinguni illi niyafanye mapenzi yangu, hali mapenzi yake aliyenipeleka.


Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?


Si kwamba mtu amemwona Baba, illa yeye atokae kwa Mungu huyu ndiye aliyemwona Baba.


Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.


Itakuwaje, bassi, mmwonapo Mwana wa Adamu akijianda huko alikokuwa kwanza?


Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.


Maana Daud hakupanda mbinguni: bali yeye mwenyewe amesema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakaepanda mbinguni? (yaani ni kumleta Kristo chini,)


Mtu wa kwanza atoka katika inchi, wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.


lililo mwili wake, ukamilifu wake akamilishae vitu vyote katika vyote.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo