Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 21:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Bassi mwanafunzi yule ambae Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Bassi Simon Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Hapo yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia ya kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa), akarukia majini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Hapo yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia ya kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa), akarukia majini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Hapo yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu akamwambia Petro, “Ni Bwana!” Simoni Petro aliposikia ya kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa), akarukia majini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Basi yule mwanafunzi aliyependwa na Isa akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana Isa!” Simoni Petro aliposikia kwamba ni Bwana Isa, akajifunga nguo yake (kwa kuwa alikuwa ameitoa), naye akajitosa baharini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Yule mwanafunzi aliyependwa na Isa akamwambia Petro, “Huyu ni Bwana Isa!” Simoni Petro aliposikia kwamba ni Bwana Isa, akajifunga nguo yake (kwa kuwa alikuwa ameitoa), naye akajitosa baharini.

Tazama sura Nakili




Yohana 21:7
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu akiwaambieni, Mbona mnafanya hivi? semeni, Bwana ana haja nae; na marra atampeleka hapa.


Mwe, bassi, mmefungwa viuno, na taa zikiwaka;


maana leo katika mji wa Daud amezaiiwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.


Kwa ajili hiyo, nakuambia, Amesamehewa dhambi zake zilizo nyingi kwa kuwa amependa sana. Nae asamehewae kidogo hupenda kidogo.


Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.


Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako.


Bassi akaenda mbio hatta kwa Simon Petro, na kwa mwanafunzi yule mwingine aliyependwa na Yesu, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.


Akiisha kusema haya, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Bassi wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana.


Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu.


Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye?


Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.


Wanafunzi wengine wakaja katika mashua (maana hawakuwa mbali ya inchi kavu, illa yapata dhiraa miateen) wakilikokota jarife lenye samaki.


Neno lile alilowapelekea wana wa Israeli, akikhubiri amani kwa Yesu Kristo (ndiye Bwana wa wote),


Bassi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.


Mtu wa kwanza atoka katika inchi, wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.


Maana upendo wa Kristo watulazimisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba ikiwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, bassi walikufa wote;


NDUGU zangu, msiwe na imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana mwenye utukufu, kwa kupendelea watu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo