Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 21:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Yesu akamwambia, Nikitaka huyu akae hatta nijapo imekukhusu nini? wewe unifuate mimi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Isa akamjibu, “Ikiwa nataka aishi hadi nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Isa akamjibu, “Ikiwa nataka aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!”

Tazama sura Nakili




Yohana 21:22
20 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.


Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha, wakinena, Tuambie, haya yatakuwa lini? Na nini dalili ya kuja kwako, na ya mwisho wa dunia?


Kwa sababu hii na ninyi mwe tayari; kwa sababu saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.


AKAWAAMBIA, Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawa wasimamao hapa ambao hawataonja mauti hatta watakapouona ufalme wa Mungu umekuja kwa nguvu.


Akasema hili kwa kuonyesha ni mauti gani atakayomtukuza Mungu. Na akiisha kusema haya, akamwambia, Nifuate.


Petro akimwona huyu, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je?


Maana killa mwulapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hatta ajapo.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?


Bassi vumilieni, ndugu, hatta kuja kwake Bwana. Mwangalieni mkulima; hungoja mazao ya inchi yaliyo ya thamani, husubiri kwa ajili yake hatta yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.


Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Illa mlicho nacho kishikeni, hatta nitakapokuja.


Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, Naam; Naja upesi. Amin: na uje Bwana Yesu.


Tazama, naja upesi; yu kheri yeye ayashikae maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo