Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 21:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Akamwambia marra ya pili, Simon wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Isa akamuuliza tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Isa akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Isa akamwambia tena, “Simoni, mwana wa Yohana, wanipenda?” Petro akamjibu, “Ndiyo Bwana, wewe unajua ya kuwa ninakupenda.” Isa akamwambia, “Chunga kondoo zangu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 21:16
18 Marejeleo ya Msalaba  

Na wewe Bethlehemu wa inchi ya Yuda, Huwi mdogo kamwe katika majumbe ya Yuda: Kwa kuwa kwako atatoka liwali Atakaewachunga watu wangu Israeli.


na mataifa yote watakusanyika mbele yake: nae atawabagua kama vile mchunga abaguavyo kondoo na mbuzi:


Akakana tena kwa kiapo, Simjui mtu huyu.


Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja illi kutafuta kilichopotea na kukiokoa.


Bassi yule kijakazi aliye mngoje mlango akamwambia Petro, Wewe nawe, je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake mtu huyu? Yeye akasema, Si mimi.


Na Simon alikuwa akisimama, anakola moto. Bassi wakamwambia, Wewe nawe je! huwi mmojawapo wa wanafunzi wake? Yeye akanena, Sio mimi.


Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


Bassi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka wafu Mchungaji wa kondoo aliye mkuu, kwa damu ya agano la milele, Bwana wetu Yesu,


Kwa maana mlikuwa kama kondoo wanaopotea; lakini sasa mmemrudia Mchunga na Askofu wa roho zenu.


lichungeni kundi la Kristo lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa khiari; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo;


Kwa maana Mwana Kondoo aliye kati kati ya kiti cha enzi atawachunga, nae atawaongoza kwenye chemcheni za inaji yenye uhayi, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo