Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 20:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mpate kuwa na uhai kwa nguvu ya jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Lakini hii imeandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Lakini haya yameandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Tazama sura Nakili




Yohana 20:31
36 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.


upate kujua usahihi wa maneno yale uliyofundishwa.


na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.


Nathanaeli akajibu, akamwambia, Rabbi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe mfalme wa Israeli.


Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele.


Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini.


Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu, na Mungu wangu.


Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu.


Amwaminiye Mwana ana uzima wa milele; na asiyemtii Mwana hataona uzima, hali ghadhabu ya Mungu inamkalia.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Huyu manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake killa amwaminiye atapewa ondoleo la dhambi.


Na kwa imani ya jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnaemwona na kumjua: na imani ile iliyo kwa njia yake yeye imempatia huyu mbele yemi ninyi nyote uzima huu mkamilifu.


Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?


Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, ni halali. Akajibu, akanena, Namwamini Mwana wa Mungu kuwa ndiye Yesu Kristo.


Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.


mkiupokea mwisho wa imani yenu, wokofu wa roho zenu.


Killa aungamae ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, nae ndani ya Mungu.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


Killa aendeleae mbele, asidumu katika ma-fundisho ya Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho ya Kristo, mtu huyu ana Baba na Mwana pia.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Thuatera andika, Haya ayanena Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho kama mwako wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo