Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 20:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Bassi akaenda mbio hatta kwa Simon Petro, na kwa mwanafunzi yule mwingine aliyependwa na Yesu, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Basi, akaenda mbio hadi kwa Petro na yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na wala hatujui walikomweka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Hivyo akakimbia kwa Simoni Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine ambaye Isa alimpenda, na kusema, “Wamemwondoa Bwana kaburini, na hatujui walikomweka!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Hivyo akaja akikimbia kwa Simoni Petro pamoja na yule mwanafunzi mwingine ambaye Isa alimpenda, na kusema, “Wamemwondoa Bwana Isa kaburini, na hatujui walikomweka!”

Tazama sura Nakili




Yohana 20:2
9 Marejeleo ya Msalaba  

Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.


Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako.


Nao wakamwambia, Bibi, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala sijui walikomweka.


Yesu akamwambia, Bibi, unalilia nini? Unamtafuta nani? Yeye, akidhani ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, kama umemchukua wewe, niambie ulipomweka, nami nitamwondoa.


Kwa maana hawajalifahamu andiko bado, kwamba imempasa kufufuka.


Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye?


Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.


Bassi mwanafunzi yule ambae Yesu alimpenda akamwambia Petro, Ndiye Bwana. Bassi Simon Petro, aliposikia ya kwamba ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana alikuwa uchi), akajitupa baharini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo