Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 20:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Yesu akamwambia, Bibi, unalilia nini? Unamtafuta nani? Yeye, akidhani ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, kama umemchukua wewe, niambie ulipomweka, nami nitamwondoa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Yesu akamwuliza, “Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, “Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Yesu akamwuliza, “Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, “Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Yesu akamwuliza, “Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Maria, akidhani kwamba huyo ni mtunza bustani, akamwambia, “Mheshimiwa, kama ni wewe umemwondoa, niambie ulikomweka, nami nitamchukua.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Isa akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?” Mariamu, akidhani alikuwa anaongea na mtunza bustani, akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nioneshe ulikomweka, nami nitamchukua.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Isa akamwambia, “Mwanamke, mbona unalia? Unamtafuta nani?” Maria akidhani ya kuwa aliyekuwa anaongea naye ni mtunza bustani, kwa hiyo akamwambia, “Bwana, kama ni wewe umemchukua, tafadhali nionyeshe ulikomweka, nami nitamchukua.”

Tazama sura Nakili




Yohana 20:15
12 Marejeleo ya Msalaba  

Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa.


Nae akawaambia, Msistaajabu; muamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa: amefufuka: bayupo hapa: patazameni pahali walipomweka.


wakadhani yumo katika msafara yao, wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao,


Nao wakiingiwa na khofu na kuinama kifudifudi hatta inchi, wakawaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hayi katika wafu? Hayupo hapa, bali amefufuka.


Wakamwambia, Rabbi (tafsiri yake, Mwalimu), unakaa wapi? Akawaambia, Njoni muone.


Bassi Yesu, akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Mnamtafuta nani? Wakamjibu, Yesu Mnazareti.


Bassi akawauliza marra ya pili, Mnamtafuta nani? Wakasema, Yesu Mnazareti.


Nao wakamwambia, Bibi, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala sijui walikomweka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo