Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 20:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA siku ya kwanza ya sabato Mariamu Magdalene akaenda kaburini alfajiri, kungali giza bado, akaliona jiwe limeondolewa kaburini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Alfajiri na mapema Jumapili, kukiwa bado na giza, Maria Magdalene alikwenda kaburini, akaliona lile jiwe limeondolewa mlangoni pa kaburi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa bado giza, Mariamu Magdalene alienda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Alfajiri na mapema siku ya kwanza ya juma, kulipokuwa kungali giza bado, Maria Magdalene alikwenda kaburini na kukuta lile jiwe limeondolewa penye ingilio.

Tazama sura Nakili




Yohana 20:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yose, na mama yao wana wa Zebedayo.


akanweka katika kaburi lake jipya, alilolikata mwambani; akafingirisha jiwe kubwa hatta mlango wa kaburi, akaenda zake.


Bassi amuru kaburi lilindwe sana hatta siku ya tatu; wasije wanafunzi wake usiku wakamwiba, wakawaambia watu, Amefufuka katika wafu: na kosa la mwisho litapita lile la kwanza.


Wakenda zao, wakalilinda sana kaburi, wakilitia lile jiwe muhuri, pamoja na wale askari walinzi.


SABATO ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, akaenda Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, kulitazama kaburi.


Na kumbe! palikuwa na tetemeko kubwa la inchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka mbinguni, akakaribia akalifingirisha lile jiwe mbali ya mlango, akaketi juu yake.


Akanunua saanda, akamshusha, akamfungia ile saanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani: akafingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.


Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba.


Bassi Yesu akiugua tena nafsini mwake akatika kaburini. Nalo lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.


Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.


Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.


Baada ya siku nane wanafunzi wake walikuwamo ndani marra ya pili, na Tomaso pamoja nao. Yesu akaja, milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani kwenu.


Hatta siku ya kwanza ya juma, wanafunzi walipokusanyika illi kumega mkate, Paolo akawakhutubu, akaazimu kusafiri siku ya pili yake, akafuliza maneno yake mpaka nsiku wa manane.


Siku ya kwanza ya juma killa mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; changizo zisifanyike hapo nitakapokuja:


Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo