Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 akaingia tena Praitorio, akamwamhia Yesu, Umetoka wapi wewe? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Basi, akaingia ndani ya ikulu tena, akamwuliza Yesu, “Umetoka wapi wewe?” Lakini Yesu hakumjibu neno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Basi, akaingia ndani ya ikulu tena, akamwuliza Yesu, “Umetoka wapi wewe?” Lakini Yesu hakumjibu neno.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Basi, akaingia ndani ya ikulu tena, akamwuliza Yesu, “Umetoka wapi wewe?” Lakini Yesu hakumjibu neno.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Akaingia tena ndani ya jumba la kifalme, akamuuliza Isa, “Wewe umetoka wapi?” Lakini Isa hakumjibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Akaingia tena ndani ya jumba la kifalme, akamuuliza Isa, “Wewe umetoka wapi?” Lakini Isa hakumjibu.

Tazama sura Nakili




Yohana 19:9
18 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Yesu akanyamaza. Kuhani mkuu akamjihu, akamwambia, Nakuapisha Mungu aliye hayi, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.


Ndipo askari wa liwali wakamchukua Yesu ndani ya praitorio, wakamkusanyia kikosi kizima.


Akamwuliza kwa maneno mengi, yeye asimjibu lo lote.


Bassi wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa hatta Praitorio; ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya Praitorio, wasije wakatiwa najis, bali waile Pasaka.


Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?


Yesu akajibu, Wewe wasema hivi kwa nafsi yako, ama watu wengine walikuambia khabari zangu?


Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.


Bassi Pilato akamwambia, Husemi na mimi? Hujui ya kuwa nina mamlaka ya kukusulibisha na nina mamlaka ya kukufungua?


Bassi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa;


Yesu akajibu akawaambia, Ningawa mimi ninajishuhudia nafsi yangu, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na niendako; lakini ninyi hamjui nilikotoka, wala niendako.


wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo