Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Makuhani wakuu na walinzi walipomwona wakapaza sauti: “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni basi, nyinyi wenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimi sikuona hatia yoyote kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Makuhani wakuu na walinzi walipomwona wakapaza sauti: “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni basi, nyinyi wenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimi sikuona hatia yoyote kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Makuhani wakuu na walinzi walipomwona wakapaza sauti: “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni basi, nyinyi wenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimi sikuona hatia yoyote kwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulubishe. Lakini mimi sioni msingi wowote wa kumshtaki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Wale viongozi wa makuhani na maafisa walipomwona, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe! Msulubishe!” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi mkamsulubishe, mimi sioni hatia juu yake.”

Tazama sura Nakili




Yohana 19:6
15 Marejeleo ya Msalaba  

Na Petro akamfuata kwa mbali hatta behewa ya kuhani mkuu, akaingia ndani, akaketi pamoja na watumishi, auone mwisho.


Pilato akawaambia, Bassi, nimtendeni Yesu aitwae Kristo? Wakanena wote, Asulibiwe.


Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.


Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu.


Bassi Yuda akiisha kupokea kikosi cha askari, na watumishi waliotoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaenda huko na makandili na taa za mkono na silaha.


Bassi Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, mkamhukumu kwa sharia yenu. Wayahudi wakamwambia, Sisi hatuna rukhusa kuua mtu;


Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani? Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake.


Bassi wale wakapiga kelele, Mwondoshe, mwondoshe, msulibishe. Pilato akawaambia, Nimsulibishe mfalme wenu? Makuhani wakuu wakajibu, Hatuna mfalme illa Kaisari.


Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake.


mtu huyu alitwaliwa nanyi kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake taugu zamani, nanyi mkamsulibisha kwa mikono mibaya, mkamwua:


Ni yupi katika manabii ambae baba zenu hawakumwudhi? nao waliwaua wale waliotabiri khabari za kuja kwake yule mwenye haki; ambae ninyi sasa mmemsaliti mkamwua;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo