Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Pilato akatokea tena nje akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa sioni khatiya yo yote kwake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Pilato akatoka nje tena, akawaambia, “Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Pilato akatoka nje tena, akawaambia, “Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Pilato akatoka nje tena, akawaambia, “Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Pilato akatoka tena nje, akawaambia wale waliokusanyika, “Tazameni, namkabidhi Isa kwenu kuwajulisha kwamba mimi sioni msingi wowote wa kumshtaki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Pilato akatoka tena nje akawaambia wale waliokusanyika, “Tazameni, namkabidhi Isa kwenu kuwajulisha kwamba mimi sikumwona ana hatia.”

Tazama sura Nakili




Yohana 19:4
16 Marejeleo ya Msalaba  

Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.


Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.


akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Pilato akawaambia makuhani wakuu na makutano, Mimi sioni khatiya yo yote katika mtu huyu.


Na sisi kweli ina haki; kwa maana sisi tunalipwa ijara ya haki ya matendo yetu: bali huyu hakutenda neno lisilofaa.


Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.


Bassi Pilato akaingia Praitorio tena, akamwita Yesu, akamwambia, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi?


Pilato akamwambia, Kweli ni kitu gani? Akiisha kusema neno hili akawatokea Wayahudi marra ya pili, akawaambia, Mimi sioni khatiya yo yote kwake.


Bassi wale makuhani wakuu na watumishi walipomwona, wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe, msulibishe. Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi, kamsulibisheni: kwa maana mimi sioni khatiya kwake.


Maana alimfanya yeye asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili vefu, illi sisi tuwe haki ya Mungu katika Yeye.


Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;


bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana kondoo asio na ila, na asio na waa, ya Kristo,


yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake;


Kwa maana Kristo nae aliteswa marra moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio baki, illi atulete kwa Mungu; mwili wake akifishwa, bali roho yake akihuishwa.


Na mnajua ya kuwa yeye alidhihiri, illi aziondoe dhambi zetu; na dhambi haimo ndani yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo