Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Yohana 19:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Naye aliyeona tukio hilo ameshuhudia ili nanyi mpate kuamini. Na hayo aliyosema ni ukweli, tena yeye anajua kwamba anasema ukweli).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Naye aliyeona tukio hilo ameshuhudia ili nanyi mpate kuamini. Na hayo aliyosema ni ukweli, tena yeye anajua kwamba anasema ukweli).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Naye aliyeona tukio hilo ameshuhudia ili nanyi mpate kuamini. Na hayo aliyosema ni ukweli, tena yeye anajua kwamba anasema ukweli).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Mtu aliyeona mambo hayo ndiye alitoa ushuhuda, nao ushuhuda wake ni kweli. Anajua kuwa anasema kweli, naye anashuhudia ili pia nanyi mpate kuamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Mtu aliyeona mambo hayo ndiye alitoa ushuhuda, nao ushuhuda wake ni kweli. Anajua kuwa anasema kweli, naye anashuhudia ili pia nanyi mpate kuamini.

Tazama sura Nakili

Yohana 19:35
15 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nafurahi kwa ajili yenn kwamba sikuwa huko, mpate kuamini: lakini na twende kwake.

Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia siku zote; lakini kwa ajili ya makutano hawa wanaozunguka nalisema haya, wapate kuamini kwamba ndiwe uliyenituma.

Na sasa nimewaambieni kabla haijawa, kusudi iwapo, mwamini.

Na ninyi pia mnashunudu, kwa kuwa tangu mwanzo mmekuwa pamoja nami.

Bassi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, akamwambia mama yake, Bibi, tazama, mwana wako.

lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.

Nasi tu mashahidi ya mambo yote aliyoyatenda katika inchi ya Wayahudi na katika Yerusalemi; ambae walimwua wakamtundika mtini.

Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.

NAWASIHI wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadae;

Nimewaandikia mambo haya, illi mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.

Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Na sisi pia twashuhudu, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo