Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Yesu alipokwisha pokea hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainamisha kichwa, akatoa roho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Yesu alipokwisha pokea hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainamisha kichwa, akatoa roho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Yesu alipokwisha pokea hiyo siki, akasema, “Yametimia!” Kisha akainamisha kichwa, akatoa roho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Baada ya kuionja hiyo siki, Isa akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Baada ya kuionja hiyo siki, Isa akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa chake, akaitoa roho yake.

Tazama sura Nakili




Yohana 19:30
28 Marejeleo ya Msalaba  

kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


Nae Yesu akiisha kupaaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.


Yesu akajibu, akamwambia, Hayo yaache sasa: kwa kuwa hivi imetupasa kutimiza haki yote. Bassi akamwacha.


Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho.


Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho.


Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu: na alipokwisha kusema haya akatoa roho.


Mimi ndimi niliye mchunga aliye mwema: mchunga aliye mwema huweka maisha yake kwa ajili ya kondoo.


Hakuna mtu aniondoleae, bali mimi nauweka mwenyewe. Nina uweza wa kuuweka, tena nina uweza wa kuutwaa tena. Agizo hili nalilipokea kwa Baba yangu.


Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza.


Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu.


Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.


Kwa maana Kristo ni mwisho wa sharia, illi killa aaminiye apate haki.


ambae Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa damu yake, kwa njia ya imani, illi aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizotangulia, katika uvumilivu wa Mungu:


Bassi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, illi mwe donge jipya, kama vule mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka yetu amekwisha kutolewa sadaka kwa ajili yetu, yaani Kristo;


tena, alipoonekana ana umho kama mwana Adamu, alijidhili, akawa mtii hatta mauti, nayo mauti ya msalaba.


tukimtazama Yesu, aliveianzisha imani yetu na kuitimiliza; ambae kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele zake aliuvumilia msalaba na kuidharau aibu, nae ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.


Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo