Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 Baada ya haya Yesu, akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizwa, andiko litimizwe, akasema, Nina kiu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Kisha, Yesu aliona kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Kisha, Yesu aliona kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Kisha, Yesu aliona kwamba yote yalikuwa yametimia; na, ili Maandiko Matakatifu yapate kutimia, akasema, “Naona kiu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Baada ya haya, akijua kuwa mambo yote yamemalizika, na ili kutimiza Maandiko, Isa akasema, “Naona kiu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Baada ya haya, Isa hali akijua kuwa mambo yote yamemalizika, alisema ili kutimiza Maandiko, “Naona kiu.”

Tazama sura Nakili




Yohana 19:28
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nina ubatizo wa kubatizwa nao, na nina dhiiki namna gani hatta utakapotimizwa!


Bassi, Yesu akawachukua wale thenashara akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemi, na yatatimizwa mambo yote aliyoandikiwa Mwana wa Adamu na manabii.


Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho.


walioonekana katika utukufu, wakanena khahari ya kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemi.


HATTA kabla ya siku kuu ya Pasaka, Yesu akijua ya kuwa saa yake imefika atakayotoka katika ulimwengu huu kwenda kwa Baba, akiwa aliwapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapeuda ukomo wa upendo.


Mimi nimekutukuza duniani. Kazi ile uliyonipa niifanye nimeimaliza.


Bassi Yesu, akijua yote yatakayompata, akatokea, akawaambia, Mnamtafuta nani? Wakamjibu, Yesu Mnazareti.


Bassi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani; andiko litimie linenalo, Waligawanya nguo zangu, na vazi langu walilipigia kura. Bassi ndivyo walivyofanya askari.


Bassi Yesu alipoipokea siki, akasema, Imekwisha: akainama kichwa, akatoa roho.


Kwa maana haya yalitukia andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena,


Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka nikaimalize kazi yake.


Hatta walipomaliza yote aliyoandikiwa, wakamshusha katika mti, wakamweka kaburini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo