Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Yohana 19:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 akatoka, akijichukulia msalaba wake, hatta mahali paitwapo pa kichwa, na kwa Kiebrania Golgotha;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Naye akatoka akiwa amejichukulia msalaba wake kwenda mahali paitwapo “Fuvu la Kichwa” (kwa Kiebrania Golgotha).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Isa, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha).

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Isa, akiwa ameubeba msalaba wake, akatoka kuelekea mahali palipoitwa Fuvu la Kichwa (kwa Kiebrania ni Golgotha).

Tazama sura Nakili




Yohana 19:17
23 Marejeleo ya Msalaba  

Nae asiyechukua msalaba wake na kufuata nyuma yangu, hanifai.


Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Wakaweka juu ya kichwa chake mshitaka wake, ulioandikwa, HUYU NI YESU, MFALME WA WAYAHUDI.


Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.


Anwani ya mshitaka wake iliandikwa juu, MFALME WA WAYAHUDU.


Kristo, mfalme wa Israeli, na ashuke sasa msalabani tupate kuona na kuamini. Nao waliosulibiwa pamoja nae wakamlaumu,


Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Na mfu ye yote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.


Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.


Hatta walipofika pahali paitwapo Kichwa, ndiko walikomsulibisha, na wale wakhalifu, mmoja mkono wa kuume, na mmoja mkono wa kushoto.


Palikuwa na anwani juu yake kwa harufi za kiyunani na kirumi na kiebrania, HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.


Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate.


Bassi Pilato, aliposikia maneno haya, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti, mahali paitwapo Sakafu ya mawe, na kwa Kiebrania Gabbatha.


Na huko Yerusalemi penye mlango wa kondoo pana birika, iitwayo kwa Kiehrania Bethesda, nayo ina matao matano.


wakamtoa nje ya mji, wakampiga mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyekwitwa Saul.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo